JINSI YA KUTENGENEZA FILAMU KWA GHARAMA NDOGO
(Zero Budget Filmmaking)
MAFANIKIO YANAPATIKANAJE?
Katiaka ulimwengu wa filamu hivi sasa, muandaaji wa filamu anaweza kuandaa filamu yake kwa gharama ndogo na ikamuingizia pesa nyingi tofauti na filamu za gharama kubwa zilizokuwa zikiandaliwa miaka iliyopita, nah ii ni kutoakana na ukweli kwamba hivi sasa gharama za uandaaji zimeshuka baada ya teknolojia mpya ya vifaa vianvyotumika kutengeneza filamu kupatikana kwa urahisi na kwa bei ndogo ambayo hata muandaaji filamau wa kawaida anaweza kuimudu. Na pia katika ulimwengu wa sasa wa filamu ni rahisi pia kufanikisha kazi ya uandaaji wa filamu kwasababu inahusisha idara nyingi zinazohitaji kufanya kazi mbalimbali kwenye filamu ili kuifanikisha, hapa nmaanisha studios, websites, traditional TV, gamers , banks, brands n.k wote hawa kazi zao zinahitaji uwapo wa filamu ili kufanikisha shughuli zao. Studios na wasambazaji, websites na television vyote hivi vina hardware kwa ajili ya kuonyeshea filamu, wanachokosa hapa ni software ambazo ni filamu zenyewe hivyo basi kama muandaaji ataanda filamu yake nzuri kwa gharama nafuu ni lazima atapata pesa kutokana na mauzo ya kawaida na pia mauzo ya kwenye makampuni haya yanayohitaji filamu ili kufanya biashara zake.
Mpenzi msomaji wa makala zangu za filamu au mdau wa filamu, nimejaribu kukufundisha jinsi unavyoweza kuandaa filamu yako kwa gharama nafuu na kuhakikisha kwamba inakupatia mamilioni ya shilingi.
- HADITHI (The Story Is Everything)
Katika filamu kwa wale wapenzi wa kuangalia filamu, hakuna kinachoweza kukufanya usichoke kuangali filamu husika zaidi ya hadithi. Kama hadithi ni nzuri na ikakushika nakuhakikishia kwamba hakuna atakaejali kama filamu imetengezwa kwa gharama kiasi gani. Hadithi ina vitu vine muhimu vinavyoweza kuifanya hadithi ikazaa filamu nzuri.
Kwanza kabisa hadithi yako lazima iwe na wahusika watakaoibeba na kuisimulia. Kitu cha pili muhimu hadithi yako inatakiwa iwe na setting! Iwe na mtiririko utakaoifanya filamu iwe filamu. Tatu, katika hadithi yako kunatakiwa kuwepo na vitendo (actions) kwa wahusika (characters) kisha kuwepo na maneno ambayo waigizaji watayatamka ( Dialogue).
Katika usimuliaji hadithi kwa mtindo wa filamu, hapa mwandishi au muandaaji wa filamu anatakiwa kuhakikisha kwamba hivyo vitu vine nilivyovitaja hapo juu havishabihani pia visionekane kwamba vinaelekeana hapa tayari filamu yako itakuwa na kitu tunachokiita (suspense)! Endapo mwandishi atafanikiwa kuvijenga vitu hivi katika filamu yake hapa kitaalamu tunasema mwandishi amefanikiwa kucheza na simulizi yake ( mastered the craft of storytelling).
- MAHALI (Locations)
Katika uandaaji wa filamu ya gharama nafuu kuna vitu vikubwa viwili ambavyo ni muhimu ambavyo ni Uoigaji picha (camera) na maeneo yatakayotumika katika upigaji picha yaani (locations). Vitu hivi viwili ni lazima vitakugharimu kwasababu kuwasafirisha wasanii na team nzima ya production kutoka location moja hadi nyingine ni gharama pia muda unapotea mwingi, hivyo hapa lazima budget yako itaongezeka. Endapo utafanikiwa kutumia location moja tu basi hapo unaweza kupunguza gharama na muda utakaoutumia katika kuandaa filamu yako. Locations zinaweza kuwa nyingi au moja lakini hii inategemea na script inavyotaka.
3.UPIGAJI PICHA (Image Capture)
Kuchagua camera inayoendana na mahitaji ya script yako ni muhimu sna kabla kazi nzima ya upigaji picha haijaanza. Siku hizi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ni rahisi kupata camera nzuri kwasababau wengi hutumia camera za dijitali (digital camera).Wakati wa kuchagua Camera yako vitu viwili muhimu unatakiwa uvizingatie navyo ni compression na lenses.Ifahamike kwamba digital camera nyingi zinafanana uwezo, kinachoweza kuongeza ubora wa picha zako ni aina na uwezo wa lenses unazotumia na idadi ya frame utakazozalisha kweny shots zako (pixels per frame) hapa utapata compression nzuri.
ITAENDELEA...
No comments:
Post a Comment