HII NDIYO SABABU YA
DIAMOND PLATNUMZ KUTOONEKANA KWENYE PARTY YA ZARI WHITE PARTY 2015 JIJINI
KAMPALA NCHINI UGANDA!
Kimenuka!
 |
Zari & Diamond Platinum |
Katika hali isiyo ya
kawaida kuhusiana na sakata la mahusiano ya kimapenzi baina ya Zari ambaye ni
mzazi mwenza wa East African Rolls Royce musician” Diamond Platnumz zamani
akifahamika kama Nasib Abdul na mtalaka wa mpenziwe huyo yaani Don Ivan
Semwanga kwamba bado hali ni tete kutokana na ukweli kwamba Ivan anaendelea
kukana kufahamu uzazi wa mototo wa nne wa bimkubwa Zarina Hassan kwamba baba wa
motto huyo ni Diamond!
 |
Rich Gang |
Hii imejirudia majuzi nchini Uganda katika tukio
lijulikanalo kama “ZARI ALL WHITE PARTY” ambapo safari hii linadaiwa kusimamiwa
na wamiliki wenyewe yaani RICH GANG kundi la matajiri wa Kiganda linaloongozwa
na mtalaka wa Zari aitwaye Ivan Semwanga. Katika kuinukisha kile kilichonuka,
Ivan alisema katika mahojiano yake na vyombo mbali mbali vya habari nchini humo
na kudai kwamba “event” hiyo ni mali ya Rich Gang na Zari huwa anatumwa
kuipamba na kuisimamia tu! Wiiki iliyopita ambapo shughuli hiyo ilichukua
nafasi jijini Kampala ambapo pia mwanamuziki Diamond Platnumz alikuwapo jijini
humo kwa shughuli zake za kimuziki lakini alizuiwa kuungana na mzazi mwenzake
yaani Zari katika shughuli hiyo kutokana na kilichodaiwa kuwa ni katazo la
Ivan! Ivan anadaiwa kumpiga mkwara Diamond kutokanyaga kwenye party hiyo na
kama angeonekana angefukuzwa kama mbwa! Bado kuna utata unaofukuta kwa muda
mrefu kuhusiana na hatma ya ndoa kati ya Zari na Ivan, umuliki wa mali zao
ambapo mara kadhaa Ivan amejitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai kwamba
Zari siyo mmiliki wa mali anazoonekana nazo bali ni msimamizi na kudai kwamba
yeye Ivan ndiye mmiliki wa mali hizo.Tusubiri
No comments:
Post a Comment