FILAMU ZINALIPA, LAKINI SERIKALI YA BONGO INABANA!
Katika
wakati kama huu ambapo hali ya maisha imekuwa ngumu, ajira hakuna hasa hapa
kwetu Tanzania, tasnia ya filamu au sanaa kwa ujumla inaweza kuwa suluhisho
pekee la kupatia ajira mamia ya watanzania hasa vijana! (The... nation, in particular, needs the sector to help rejuvenate hope
of better time and faith in the land's ability to ultimately come out of the
woods).
“This is my
thinking” mimi kama Selles Mapunda, hizo ndizo fikra zangu! Lakini situation
hapa nchini kwetu haiku hivyo hasa kwetu sisi wadau wa tasnia hii ya filamu. Serikali
yetu chini ya maraisi wote waliopita mpaka leo hii JK haitusaiidii katika
misingi inayoweza kutengeneza ajira kwa wasanii. Hapa namaanisha kwamba
serikali kujenga misingi itakayo wasaidia wasanii wote sio wale wawili watatu
wanaoitwa kwenye kampeni za uchaguzi au wale walio karibu na raisi! Hapa naweza
nikasema kwamba mh. Raisi JK na serikali yenu mnaiweka tasnia ya filamu kwenye
“situation where the country tends to
exploit and wreck the filmmakers' investments without propping them” .
Nilibahatika
kufanyiwa interview na mwandishi wa habari za mambo ya filamu za kiafrika toka
nchini Marekani kupitia kwenye televisheni ya Chanel ten ya hapa nchini, mimi
kama Director na Producer, mwandishi huyu
alitaka kujua nini sisi waandaaji wa filamu wa hapa Tanzania tunafanya kwenye
tasnia hii ya filamu hasa katika kipengele cha “Telling stories in a Tanzanian way
about culture and creativity”. Alitaka pia kufahamu filamu zetu
zinasaidiaje katika kuwajenga watanzania katika kukuza na kuendeleza mila na
desturi za mtanzania, niliongea nae mambo mengi sana lakini moja kati ya mambo
makubwa niliyojifunza kwake ni kwamba tasnia ya filamu hapa nchini kama itapata
sapoti kutoka serikalini inaweza pia kubadilisha maisha ya watanzania wengi
hususani wasanii aliniambia “Bongo movies
can be used to solve society's problems, can launch a man from grass to grace”.
Interestingly,
mimi binafsi kama director na mshikadau wa Bongo Movies nikavuta picha ya
nilikotoka mpaka nilipo kwenye hii tasnia, tangu utoto wangu nilikuwa na
mapenzi na tasnia hii, rasmi nilianza kujishughulisha na mambo ya tasnia ya
filamu nikiwa na umri wa miaka 14 wakati huo wenzangu wengi walikuwa bado
wanabebwa mimi tayari nilikuwa nafuatilia tamthilia za Isidingo na Days of our
lives!
“Nilianza kuigiza nikiwa shule ya msingi miaka
ya 80, katika umri huo! Baba yangu hakupenda kabisa mwanawe ajiingize kwenye
mambo ya uigizaji au mambo ya sanaa kwa ujumla. Nakumbuka alithubutu kumwambia
mama yangu kwamba hataki mwanawe yeyote ajiingize kwenye mambo ya sanaa na hata
mambo ya uandishi wa habari na utangazaji, yeye alikuwa siku zote anasema
kwamba “artists, journalists and
broadcasters do not maintain stable families as they never had the time to
spend with their families”.
Hivyo basi
alijitahidi kutulazimisha tusome fani nyingine tofauti na sanaa na uandishi wa
habari. Kwa bahati mbaya mimi nilipomaliza kidato cha nne, nikajiunga na kidato
cha tano na sita nilikosoma combination ya HGL (History, Geography & Language) na baadae kujiunga na chuo
kikuu cha UDSM kwenye faculty a Sociology. Mzee Mapunda alijitahidi sana kwa
watoto wake wote lakini kwa bahati mbaya kuna usemi wazungu wanapenda sana
kuutumia wanasema kwamba “one cannot live
out of one's calling and one cannot leave out what one has seen. It is an
in-built thing”. Kwamba kufanya shughuli za filamu na uandishi iko kwa damu
yangu (is in my blood stream) Hivyo
basi kwa mapenzi yangu ya mambo ya sanaa nikaamua kujisomesha mwenyewe kwenye
chuo cha sanaa UNILAG kitivo cha uandishi, uongozaji na uzalishaji filamu
nchini Nigeria.
Kwa hakika
naweza sema kwamba “Im within my line of calling” Yes, kufanya filamu kwangu ni wito, na
ukiangalia leo hii mimi ni mmoja kati ya wadau wakubwa kwenye tasnia ya filamu
hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Mimi ni filmmaker ambae nina taaluma ya
uandishi wa miswada ya filamu na uongozaji (writing, and directing) mpaka
ninaandika makala hii nimejifunza mambo mengi sana kwenye tasnia hii hususani
hapa Tanzania, Nigeria na Ghana. Mwisho wa yote nimegundua kwamba ili
kuiendeleza tasnia hii ni lazima wadau tufanye mapinduzi kwa kutengeneza filamu
zenye ubora wa kimataifa ili kuzifanya kazi zetu zitambulike kimataifa. (only way we can make an impact in the movie
industry is to produce quality films that will bring change).
Nimefanya
kazi ya kuandika na kuongoza filamu zaidi ya 30 kupitia kampuni ya usamabazaji
wa filamu iitwayo Steps Entertainment ltd, lakini kuna vitu ambavyo kwa kiasi
kikubwa kampuni haikuzingatia kuhusu ubora wa filamu inazoandaa na hata
kusambaza, nah ii ni kwa sababu kampuni kazi yake kubwa ni kufanya biashara ya
kusambaza filamu na sio kuandaa hivyo basi kwa kuliona hili nikaamua rasmi
kuanza kuandaa filamu zangu binafsi. Nikaamka tu na kujitamkia kimoyomoyo
kwamba “I have to produce my own movies, I
have to produce movies for people. I have to direct movies. And, I ran away
from those things”. Nafsini
niligundua kwamba namna pekee ya kufanya mabadiliko ni kuandaa filamu zangu kwa
kiwango ambacho wapenzi wa filamu hapa Tanzania, Afrika na duniani kote
wataelewa ninachokifanya! Nilijiangalia
mwenyewe, nikazipima akili, uwezo na ujuzi nilionao kwenye mambo ya uandaaji wa
filamu “it occurred to me that the only
way I can make that impact is to produce quality films”.
(story ndiyo kwanza
imeanza,unataka kujua nimeandika na kuongoza filamu zipi? Nimefanya kazi na
wasanii gani? Usikose sehemu ya pili ya makala hii)
No comments:
Post a Comment