wembe ads

wembe ads

Search Posts

Tanzania's Number one gossip blog with latest entertainment news, scandals, fashion and videos. contacts +255 789 120 888 (Dar Es Salaam, Tanzania)

Tuesday, 22 December 2015

SHILOLE AANGUKIA KWA SELEBOBO!


Mwanamuziki machachari na mwenye vibweka nchini Tanzania Zuwena Mohamed a.k.a Shilole kiuno anayefanya vizuri na wimbo wake wake wa nyang’anyang’a ameangukia kwa producer maarufu nchini Nigeria na Afrika kwa ujumla aitwaye Udoka Chigozie Oku  a.k.a Selebobo imefahamika. Nyeti hizo zimetua kwenye dawati la Kachumbari blog Jtatu ya tarehe 21-12-2015 moja kwa moja kutoka jijini Lagos nchini Nigeria ambako msanii huyo (Selebobo) ambae ndiye aliyetengeneza nyimbo kali kama vile Ada Ada" ya msanii Flavour, YOYO remix aliyomshirikisha nguli J. Martins, "Balance For Me" ya msanii Dipp na  "Johnny" ya msanii Yemi Alade, anaendesha studio yake ya shughuli za muziki. Akilivutia waya dawati letu Shilole alitanabaisha kwamba katika kuboresha kazi zake ameona producer huyo mnaijeria anavyo vionjo vya muziki anaoufanya yeye hivyo anaamini kwa kufanya kazi nae atakuza na kuuboresha muziki wake. Hivi sasa Shilole yuko ndani ya studio jijini Lagos akipika wimbo mpya ambao hakuutaja kwa jina. Inshalah, Kachumbari ya Moto inamtakia yote yenye kheri katika kazi zake.
Selebobo


No comments:

Post a Comment