MASOGANGE AWAPIGA CHANGA LA MACHO WATU KUHUSU DAVIDO!
![]() |
Agnes Masogange |
Mwanadada muuza sura kiboko sana
nchini Tanzania anayekwenda kwa jina la Agnes Masogange amekanusha kuwa na
ujauzito wa msanii nguli wa muziki toka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke
‘Davido’, akifungukia ishu hiyo bint huyo anayesifika kwa figa matata amesema
“Hivi unajua mimi nashangaa sana kuhusu maneno ya mimi na Davido! Anawezaje
sasa kunipa mimba jamani wakati hatuna uhusiano wa kimapenzi? Hiyo mimba
inapitia wapi? Watu wanahisi tu kwamba nina uhusiano na Davido lakini siyo
kweli na hakuna mwenye uhakika kuhusu hilo,” alisema Masogange.
![]() |
David Adedeji Adeleke ‘Davido' |
Pamoja nalo pia
Masogange aliweka wazi kwamba yeye anamtu wake anayeshirikiana nae kimapenzi na
siyo Davido. Licha ya Masogange kunanusha habari hiyo lakini dawati la
Kachumbari lina data zenye uhakika kwamba Masogange anatoka kimapenzi na
Davido. Tusubiri tuone!
No comments:
Post a Comment