Msanii zilipendwa wa muziki wa kizazi kipya Rehema Chalamila a.k.a Ray C ambaye alipoteza muelekeo ya kazi na maisha yake ya kimuziki baada ya kubobea katika matumizi ya madawa ya kulevya amerejea tena katika lindi hilo! Habari zenye uhakika zilizotua katika dawati la Kachumbari zinadai kwamba hivi sasa Ray C hashikiki kabisa na anaelekea kuzidiwa na madawa! Hivi karibuni Ray C amefikia hatua ya kulilia auze nyumba ya mama yake ili aende kuishi Marekani anakodai kwamba kuna wazungu wa unga wenzake! Mara ya kwanza alipobobea kwenye utumiaji wa madawa raisi mstaafu chakaramo JK Kikwete alijitolea kumsaidia kupata matibabu ambayo yalimrejesha kwenye utu lakini hakuzuchukua muda akarudia tena! Ray C, usicheze na maisha yako kwani bado watanzania wanakuhitaji!
|
No comments:
Post a Comment