RICHARD WA BBA 2 AREJEA TANZANIA!
Mshiriki na mshindi wa shindano la Big Brother Africa season 2 Rchard
Bezadenhout ambaye anaishi nchini Canada anarejea rasmi nchini Tanzania kwa
ajili ya kufanya shughuli za filamu. Akiongea hayo meneja na msemaji wa msanii
huyo Selles Mapunda amesema kwamba wakati akiwa nchini Canada Richard alijikita
katika kusomea mambo ya uandaaji filamu na sasa ameshahitimu hivyokumuwezesha
kufanya filamu zenye kiwango cha kimataifa. Aidha Mapunda aliongezea kwamba
msanii wake huyo tayari ameshafanya filamu kadhaa nchini Canada
zitakazosambazwa hapa nchini hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment