Wasanii wababaishi na wabishi katika tasnia ya filamu hapa nchi Wema Sepetu na Kajala Masanja hatimae wamepatana baada ya ugomvi uliodumu zaidi ya miaka miwili. Wasanii hao waowahi kuukoleza urafiki wao baada ya Kajala kuhukumumiwa kifungo au kulipa faini kutokana na kesi ilikuwa ikimkabili na ambayo pia ilimsotesha rumande kwa muda mrefu hakuamini macho yake pale msanii mwenzake Wema Sepetu alipoonyesha uthubutu wa kumlipia faini yote papo kwa papo na kumfanya aondokane na adhabu ya kifungo! kutokana na tukio hilo la kihistoria Kajala alithubutu kuchora tatoo yenye jina la Wema Sepetu kama shukrani. Haikuchukua muda wawili hao walimwagana na kuchukiana kama pka na panya kisa kikidaiwa kunyang'anyana wanaume! Hii leo habari zenye uhakika zimethibitisha mabint hao kusameheana na kurejesha urafiki wao tukio ambalo linadaiwa kusimamiwa na msanii mwenzao Aunty Ezekiel katika hotel ya Collesium. Kachumbari blog inawatakia kila lenye kheri katika mwanzo mpya wa urafiki wao!
No comments:
Post a Comment