wembe ads

wembe ads

Search Posts

Tanzania's Number one gossip blog with latest entertainment news, scandals, fashion and videos. contacts +255 789 120 888 (Dar Es Salaam, Tanzania)

Tuesday, 5 January 2016

CHUCHU NA JOHARI BIFU UPYAAA!
Mgogoro ulikwisha poa kitambo kati ya wasanii wa tasnia ya filamu hapa nchini Blandina Chagula a.k.a Johari na Chuchu Hans umelipuka tena! Awali mgogoro huo unaodaiwa ni wa kumgombea bwana ambaye pia ni msanii mwenzao Ray (Visent Kigosi) ulipozwa na Ray mwenyewe baada ya kutamka wazi kwamba hana mapenzi na Johari na mapenzi yake amehamishia rasmi kwa msanii Chuchu hivyo kumfanya Johari awe mpole. Lakini habari tulizonazo na zenye uhakika ni kwamba katika siku za hivi karibuni Ray amepunguza mapenzi kwa Chuchu jambo ambalo liko wazi hata kwa Johari na kupelekea Johari kutamka wazi wazi kwamba anaamini bado Ray anamuhitaji na wakati wowote yeye Johari akimuhitaji Ray anamchukua kiulaini! Maneno hayo yamechochea moto kwa Chuchu ambae nae amedai kumunyoosha Johari endapo ataendelea kumuingilia katika anga zake.

No comments:

Post a Comment