Katika hali ambayo imeshtua wengi mapema wiki hii ni pale ambapo mamia ya wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa "Team Diamond" kuzusha uzushi kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Instagra, Facebook na tweeter wakidai kwamba gari aina ya Range Rover "Evoque" alilojizawadia msanii mwenye vibweka kuliko wote tanzania Wema Isaack sepetu kwamba siyo lake na alilikodi tu kutoka kwa kijana tajiri wa madini Marleydollars kwaajili ya ku-show off! Baada ya habari hizo kuzagaa mitandaoni Kachumbari blog ilimsaka aliyedaiwa kumiliki gari hilo ambapo alikanusha na kuweka wazi kwamba Wema alikwisha linunua gari hilo kabla ya siku yake ya birthday kwa pesa taslim na kwamba ni mali yake halali.
No comments:
Post a Comment