MR. BLUE, DIAMOND NA AFANDE SELLE WAGOMBEA UNYAMA!
Msanii zao la kizazi kipya nchini Henry Samir a.k.a Mr Blue amelalama kwamba msanii mwenzake Diamond Platnumz anapenda kum-copy katika harakati zake! Akilalama kuhusiana na sakata hilo Blue alisema Diamond siyo mbunifu! Diamond anapenda kusubiri mimi nitoe idea ya kitu ndipo nae aige! Awali inadaiwa Diamond kutoka na msanii Wema Sepetu baada ya kuwa tayari Mr Blue alikwisha toka nae. Kisha Mr Blue anadaiwa kumtungia wimbo Wema Sepetu naye Diamond akafanya hivyo! Akafuatia msanii Najma aishiye nchini marekani ambapo baada ya Diamond kufahamu uhusiano wa kimapenzi kati ya Naj na Mr Blue naye pia akatembea nae na hivi sasa mr Blue anadai kujiita Simba miezi saba iliyopita na siku chache zilizopita Diamond nae akajiita Simba! Katika hali isiyo ya kawaida nae msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini Afande Sele ameingilia kati sakata hilo na kudai kuwa yeye ndiye simba dume na hao wengine wote ni "cubs"!
No comments:
Post a Comment