MATUKIO YALIYOJIRI NDOA YA WASTARA
Msanii wa filamu hapa nchini Wastara Juma amefunga ndoa kwa mara nyingine
na Mh. Mbunge wa Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma iliyofungwa Alhamisi
iliyopita, kuna matukio ya kustaajabisha.
Ndoa hiyo iliyofungwa kimyakimya, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita
nyumbani kwa mwigizaji huyo, Tabata-Barakuda, jijini Dar ambapo ilihudhuriwa na
watu wachache tofauti na ilivyotarajiwa kutokana na umaarufu wa wanandoa hao.
NDOA ILIFUNGWA KWA SIMU
Imebainika kuwa, awali ndoa hiyo ilikuwa ifungwe saa kumi jioni na
baadaye kuelezwa ilisogezwa mbele hadi saa 12 jioni, hata hivyo haikufungwa
muda huo baada ya bibi harusi kuchelewa kufika akitokea saluni alikoenda
kupambwa na kulazimika shehe afungishe ndoa hiyo kwenye simu wakati Wastara
akiwa kwenye foleni barabarani.
BWANA HARUSI AGOMA KUPIGWA PICHA
Imeelezwa kuwa, baada ya bwana harusi kutinga na wapambe wake alitoa onyo
kali huku likisisitizwa na wapambe wake kuwa hairuhusiwi kupiga picha na kutuma
kwenye mtandao wowote wa kijamii kwa vile ndoa hiyo ilikuwa ya siri.
AGOMA
KUMFUNUA BIBI HARUSI
Katika hali ya kushangaza, baada ya bibi harusi kuwasili aliingizwa
katika chumba maalum kwa ajili ya kumsubiri mumewe na hata alipoingia ndani,
shehe alimuomba amfunue mkewe ili kumhakikisha kama ndiye yeye kitu ambacho
alikipinga na kudai hakuwa na shaka naye na kuomba waendelee na kitu kingine.
No comments:
Post a Comment