RICHARD KIBOKO KABISA!
Aliyekuwa
mshindi wa shindano la Big Brother Africa season 2 ambae kwa sasa anafanya
maisha yake nchini Canada Richard Bezuidenhout amejibu mapigo baada ya mkewe
kutishia kuivunja ndoa yake kutokana na kile kilichodaiwa kusambaa kwa picha
chafu zinazoashiria uwepo wa mahusiano kati ya mshindi huyo wa zamani wa
shindano la big Brother Africa pamoja na wanawake kadhaa. Richard ambae pia ni
bonge la msanii wa filamu aliyewahi kuwika hapa nchini na filamu kibao ameamua
krudisha majeshi yaani kuondoka nchini humo na kurejea hapa nchini Tanzania.
Richard amekaririwa akisema kwamba ameona bora aonyeshe kwa vitendo kile
kilicho kilichopelekea mgoror katika ndoa yake. Akifafanua hilo Rich alisema
ameamua kurudisha majeshi hapa nchini ili kuendelea na shughuli zake za filamu
ili watanzania waone uwezo wake ulivyokuwa akimaanisha ni tofauti na hapo awali
ambapo alikuwa akiigiza bila taaluma ya fani hiyo ambapo kwa kuanzia
ameshakamilisha filamu ya Kiswahili nchini Canada inayokwenda kwa jina la “Mwanaume
siyo ATM Machine” ambayo inatarajia kusambazwa hapa nchini Tanzania hivi
karibu.
No comments:
Post a Comment